Monday, September 10, 2012

WAANDISHI WAMENANGWA NA TUNDU LISU, TUSUBIRI TAMKO


Na Hamis Shimye
TAALUMA ya uandishi wa habari nchini kila kukicha imeendelea kudharauliwa na wanasiasa na baadhi ya viongozi ambao wanajiona taaluma zao ndio bora na zenye uwezo wa kuhoji na kuakisi mambo.

Mfumo huo umeendelea kuota mizizi huku hata zile klabu, majukwaa na mabaraza ya uandishi wa habari yakiwa kimya na badala yake kuzungumzia mambo mengine ambayo hayana faida kwa mwandishi wa habari.

Uandishi wa habari Tanzania unakumbukana na changamoto lukuki ambazo zilipaswa kuwa sehemu ya mjadala kwa vyama vilivyopewa dhamana ya kuwaongoza waandishi wa habari ambao maisha na mfumo wa kazi zao umekuwa kama mchezo wa bahati nasibu.

Kitendo ambacho kinafanya thamani na hadhi ya mwandishi kila kukicha kupotea huku majina ya dharau nayo yakizidi mara 'watu wamshiko', 'makanjanja' au 'vihiyo'. Yote haya yanasababishwa na ubinafsi  na ukasuku wa kukariri matamko.

Kauli ya kashfa na Mbunge Tundu Lissu (Singida Mashariki - CHADEMA) kuhusiana na wajumbe wa tume walioteuliwa na serikali kuhusiana na kifo cha Mwandishi wa habari Daud Mwangosi kuwa baadhi yao hawana uwezo ni fedheha kubwa kwa wajumbe hao na tasnia nzima.

Mbunge huyo aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa chama chake kutokuwa na imani na tume hiyo hasa kutokana na kuwa na wajumbe baadhi aliodai wasiokuwa na ueledi wa mambo wanaochunguza.

Katika mkutano huo, Lissu alizungumza mambo mengi juu ya tume hiyo, lengo likiwa kuaminisha umma kuwa tume hiyo haifai na ndiyo maana chama chao wanaikataa huku akitaja majina ya wajumbe wa tume hiyo ambayo kimtazamo wake yeye anasema hawana uwezo.

Hata hivyo, muktadha wa hoja hii hautakuwa kuzungumzia uwezo wa kila mjumbe ndani ya tume hiyo, bali ni udhaifu wa vyama vyetu ambavyo navyo vinapotezwa katika mlengo wa kusimamia maslahi ya waandishi na kuanza kuwa watoa sauti ya wanasiasa kushindana kuikataa tume.

Kuchaguliwa kwa Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Stephen Ihema na wajumbe wengine wakiwemo mahiri katika tasnia ya habari kama Theopil Makunga (Jukwaa la Wahariri) na Pili Mtambalike (Baraza la Habari Tanzania) ilikuwa ni sehemu ya waandishi na klabu za habari kufurahia na kuipongeza serikali.

Kufurahia huko kunatokana na kifo cha Mwangosi ambaye ni mwenzetu kuwa kinachunguzwa na waandishi wenyewe, hivyo kutolewa kwa kauli za dharau kuwa waandishi wa habari hawawezi kuchunguza kifo ni tusi kubwa ambalo lilipaswa kukemewa na si kuachwa kama inavyotaka kufanywa.

Nakumbuka katika jali ya MV Bukoba, mmoja wa wana habari mahiri nchini Jenerali Ulimwengu alikuwa mjumbe wa tume iliyochunguza chanzo cha ajali hiyo. Mbona mambo yalikwenda sawa au kwa kuwa Lissu alikuwa hajapata umaarufu?

Japokuwa katika suala zima kuhusiana na tukio hilo waandishi walitofautiana kimtazamo na kifikra, lakini linapokuja suala la kudharauliwa, tunapaswa kuwa pamoja na kukemea. Kinyume chake baada ya kunang'wa na Lissu tunatakuja kupewa tusi kubwa zaidi.

Mwenye uwezo na ueledi wa kuchunguza kifo si mwanasheria pekee? Lisu anapaswa kutambua hilo na kuachana na mawazo ya Mfalme Jua,  juu ya kile anachokiamini kuwa ni sahihi na hapaswi kupingwa au kukatazwa na mtu.

Jamii inaelimishwa na kufundishwa kupitia mifumo tofauti ya maisha na ndiyo maana wanasaikolojia wanaamini tabia ya mtu ni rahisi kuifahamu kupitia matamshi na matendo yake kuwa ni makuzi gani aliyapata utotoni.

Sitaki niamini kuwa klabu, jukwaa na hata baraza lenyewe halijasikia maneno ya kejeli ya Lissu, bali naamini yapo makundi ndani ya waandishi wa habari likiwemo la wale walio tayari kwa lolote ili mradi wawanufaishe wengine na hasa wanasiasa au watwana wao.

Hilo litapongezwa kwa matamko au hata kwa kujitokeza na kusukuma magari yao kuwa hawa kwa mtazamo wao kuwa hao ni mashujaa na wazalendo wa nchi hii .

Hivyo, ningetamani nguvu iliyotumika kutoa tamko la kuwataka polisi wakae meza moja na CHADEMA kumaliza tatizo, ingetumika kutoa tamko juu ya dharau ya Lissu na chama chake kwa waandishi wa habari nchini.

Mchina Mbaroni Kwa Kuchimba Madini Kwenye Pori La Akiba.


Mtambo wa kuchimbia madini ambao Raia wa China walikamatwa wakiutumia katika pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkansi kinyume cha sheria.Raia huyu wa china amehukumiwa kulipa faini na kuamriwa kuondoa mtambo huo katika pori hilo.

Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.

 Na:  Veronica Kazimoto – MAELEZO
 Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba  madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya,  mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine  aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu  cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.

Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.

Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi  kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba. Aidha  Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.

Chaoxian Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai 25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa huru.

Saturday, September 8, 2012

KENETH SIMBAYA AULA TENA UTPC JANE MIHANJI AWA MAKAMU WAKE


Rais wa UTPC Keneth Simbaya akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa tena

Makamu wa Rais Jane Mihanji akijieleza kabla ya kuchaguliwa kwa kura za kishindo






KENETH SIMBAYA amepitishwa tena kwa kishindo katika nafasi ya Rais wa Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) hiyo baada ya kupata kura 60 kati ya Jane Mihanji amepata kura za hapana 2 na kura za ndio 60 kati ya kura 62 zilizopigwa katika uchaguzi huo.

Waandishi wa mtandao huu kutoka Dar es Salaam Esther Macha na Abdulaziz Video wanaripoti kuwaKatika uchaguzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam  Simbaya amepata kuwashukuru wajumbe kwa ushirikiano mkubwa ambao amepata kuuonyesha katika kipindi kilichopita na hivyo kuwaomba ushirikiano huo uzidi katika kipindi kichacho.

Simbaya amewataka wajumbe hao mkutano huo kuendelea kushikamana zaidi na kuwa katika uongozi wake uliopita amepata kuwa kiunganishi kizuri kati ya UTPC na wahisani kwa asilimia 150 na kuahidi kuendelea kufanya hivyo katika kipindi kijacho.

Alisema kuwa ili kuweza kusonga mbele zaidi bado UTPC inahitaji viongozi wenye mahusiano mema na wahisani ili kuiwezesha UTPC kufanya vema zaidi.

MWENYEKITI WA MBEYA PRESS KLABU CHRISTOPHER NYENYEMBE ACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA BODI YA UTPC


Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe akiomba kura katika nafasi ya ujumbe wa bodi ambayo amepita kwa kura 33 kati ya 64 zilizopigwa

Bodi Ya Mikopo Yatafuna Fedha Za Wanafunzi

 Financial statement inayoonyesha kiwango anachodaiwa wakati fedha hizo hazikulipwa na mwanafunzi huyu bado anadaiwa na chuo na kimeshikilia vyeti vyake
 Barua ambayo chuo kiliandika kuonyesha kuwa fedha zilirudishwa bodi baada ya kuwa hazikusainiwa na wanafunzi.na kuwa fedha ya mwaka wa pili haikulipwa kabisa na bodi ya mikopo
 Baada ya kufuatilia suala lake,alilifikisha hadi wizara ya elimu,na wizara ikawaandikia bodi kutaka kujua ukweli wa madai haya,Barua hii haikujibiwa
Baada ya bodi kutojibu barua ya kwanza,wizara iliandika tena kuulizia suala hilo,Hadi sasa bado bodi haijajibu kitu.

Bodi ya mikopo,inalalamikiwa kutafuna fedha za mwanafunzi MWESIGA CHRISTIAN MICHAEL aliyehititimu DUCE mwaka 2011.
 
Bodi inaonekana hawakulipa ada yake ya mwaka wa kwanza na wa pili,bali walilipa ya mwaka wa tatu pekee.
 
Alipokuwa akifuatilia akiwa bado chuoni alikuwa akiambiwa hakuna tatizo na ada zote zitalipwa.
 
Bali amejikuta akidaiwa na chuo ada ya miaka 2 zaidi ya milion 2 na chuo kimezuia vyeti vyake.Bodi ya mikopo ambayo aliingia nayo mkataba sasa inasema haimtambui na bajeti yake haipo tena.
 
Hata hivyo uchunguzi umegundua kuna udanganyifu kwa upande wa bodi kwani financial statement waliyotoa inaonyesha amelipiwa ada.
 
Isipokuwa mjengwablog,imegundua kuwa bodi,ama watumishi wake walighushi kwa makusudi na kubadili majina ya mnufaika na kulipa mtu hewa kwa miaka 2,ila wakalipa mtu stahiki mwaka wa tatu pekee.Ajabu hata hivyo,Mwesiga Christian Michael,hakunufaika na fedha hizo,bado anadaiwa na chuo na vyeti vyake vimezuiwa.Ajabu ni kuwa inaonekana anadaiwa zaidi ya milioni 7 wakati hazikulipwa fedha hizo.
 
  Ni wazi kuna udanganyifu na au wizi kwenye bodi ya mikopo,na mjengwablog imeshindwa kujua ni vipi bodi imekaidi kujibu barua za wizara mara mbili juu ya madai ya Mwesiga.

Tunadhani wenye kuhusika watafutwe na mamlaka husika ili wawajibike kwa wizi walioutenda.Hadi sasa Mwesiga hajapata ajira kwa sababu hana vyeti vya shahada.

Wednesday, September 5, 2012

Magazeti Leo Alhamisi










BAADHI YA MITAA YA MJI WA SUMBAWANGA, "SUMBAWANGA NG'ARA" YALETA MABADILIKO YA USAFI KATIKA MJI HUU

MKUU WA MKOA WA RUKWA AMUOMBA MKURUGENZI WA SUMATRA KUFANYA UKAGUZI WA MARA KWA MARA WA MELI KUEPUSHA AJALI

 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi wa SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu Peter Lupatu ambaye yupo Mkoani Rukwa kwa ajili ya ukaguzi wa bandari ya Kasanga na vifaa vya usafiri wa majini katika ziwa Tanganyika ikiwemo meli ya Mv Liemba na Mv Mwongozo. Mkuu huyo Mkoa alimuomba Mkurugenzi huyo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya majini hususani Meli ili kuepusha ajali mbaya zinaweza kujitokeza kama ilivyotokea kwa meli za Mv Spice Islanders na Mv Skagit katika bahari ya Hindi. Alisema ajali nyingi husababishwa na ubovu wa vyombo hivyo ambavyo vinahitaji ukarabati wa mara kawa mara.
Kushoto ni Meneja wa SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu D.B Mukasa, Mkurugenzi wa SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu Peter Lupatu na kushoto ni Afsa Mkuu wa Sumatra Mkoa wa Rukwa Chambo Ghadafi wakijadili mambo muhimu kuhusu sekta ya bandari na usafiri majini katika ziwa Tanganyika na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya. Miongoni mwa mambo waliyogundua kwenye ukaguzi wao ni pamoja na Meli kusafirisha abiria bila kutumia tiketi jambo ambalo wameshauri utaratibu huo ubadilike na abiria kukatiwa tiketi na kutambuliwa ili tatizo lolote likijitokeza iwe rahisi kulishugulikia.
 
Mkoa wa Rukwa unapakana kwa karibu sana na Nchi za Kidemeokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia ambapo mpaka wa nchi hizo upo katika ziwa Tanganyika. Kwa kuona umuhimu wa kuziunganisha nchi hizo kibiashara Serikali imeamua kujenga bandari ya Kasanga ambayo itakuwa kiunganishi kikubwa cha kibiashara na nchi hizo. Sio bandari peke yake bali pia barabara za lami kutoka Mkoa wa Mbeya (Tunduma)-Sumbawanga hadi Kasanga ilipo bandari hiyo inaendelea kujengwa na inategemewa kukamilika mwakani 2013. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)