Saturday, September 8, 2012

Bodi Ya Mikopo Yatafuna Fedha Za Wanafunzi

 Financial statement inayoonyesha kiwango anachodaiwa wakati fedha hizo hazikulipwa na mwanafunzi huyu bado anadaiwa na chuo na kimeshikilia vyeti vyake
 Barua ambayo chuo kiliandika kuonyesha kuwa fedha zilirudishwa bodi baada ya kuwa hazikusainiwa na wanafunzi.na kuwa fedha ya mwaka wa pili haikulipwa kabisa na bodi ya mikopo
 Baada ya kufuatilia suala lake,alilifikisha hadi wizara ya elimu,na wizara ikawaandikia bodi kutaka kujua ukweli wa madai haya,Barua hii haikujibiwa
Baada ya bodi kutojibu barua ya kwanza,wizara iliandika tena kuulizia suala hilo,Hadi sasa bado bodi haijajibu kitu.

Bodi ya mikopo,inalalamikiwa kutafuna fedha za mwanafunzi MWESIGA CHRISTIAN MICHAEL aliyehititimu DUCE mwaka 2011.
 
Bodi inaonekana hawakulipa ada yake ya mwaka wa kwanza na wa pili,bali walilipa ya mwaka wa tatu pekee.
 
Alipokuwa akifuatilia akiwa bado chuoni alikuwa akiambiwa hakuna tatizo na ada zote zitalipwa.
 
Bali amejikuta akidaiwa na chuo ada ya miaka 2 zaidi ya milion 2 na chuo kimezuia vyeti vyake.Bodi ya mikopo ambayo aliingia nayo mkataba sasa inasema haimtambui na bajeti yake haipo tena.
 
Hata hivyo uchunguzi umegundua kuna udanganyifu kwa upande wa bodi kwani financial statement waliyotoa inaonyesha amelipiwa ada.
 
Isipokuwa mjengwablog,imegundua kuwa bodi,ama watumishi wake walighushi kwa makusudi na kubadili majina ya mnufaika na kulipa mtu hewa kwa miaka 2,ila wakalipa mtu stahiki mwaka wa tatu pekee.Ajabu hata hivyo,Mwesiga Christian Michael,hakunufaika na fedha hizo,bado anadaiwa na chuo na vyeti vyake vimezuiwa.Ajabu ni kuwa inaonekana anadaiwa zaidi ya milioni 7 wakati hazikulipwa fedha hizo.
 
  Ni wazi kuna udanganyifu na au wizi kwenye bodi ya mikopo,na mjengwablog imeshindwa kujua ni vipi bodi imekaidi kujibu barua za wizara mara mbili juu ya madai ya Mwesiga.

Tunadhani wenye kuhusika watafutwe na mamlaka husika ili wawajibike kwa wizi walioutenda.Hadi sasa Mwesiga hajapata ajira kwa sababu hana vyeti vya shahada.

No comments:

Post a Comment