WATOTO yatima waliopelekwa kulelewa katika kituo cha Hospitali ya Igogwe iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamebainika kuwa wametelekezwa na walezi na wazazi waliowapeleka katika kituo hicho.
Akielezea masikitiko yake kuhusu kutelekezwa kwa watoto hao, Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Chieffoda Fungo alisema kuwa kitendo cha walezi na wazazi hao kufanya hivyo na kushindwa kutoa kutoa sh.5000 kwa mwezi kwa ajili ya matunzo kunafanya kazi ya kuwatunza kuwa ngumu.
Kiongozi huyo alisema hayo juzi wakati alipokuwa mgeni rasmi wa changizo maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya maandalizi ya jubilee ya miaka 50 tangu kwa hospitali hiyo maalumu ya misheni ambapo zaidi ya sh milioni 20 zilipatikana ikiwa ni pamoja na ahadi.
Alisema baada ya kutembelea katika kituo hicho alisikia uchungu kupata taarifa kuwa wapo baadhi ya kinababa ambao walifiwa na wake zao na hivyo kutokana na kutokuwa na walezi wengine kuamua kuwapeleka watoto hao katika kituo hicho na kisha kukimbia majukumu kwa kushindwa hata kutoa sh.5000 kwa mwezi kiasi kilichopangwa na kama mchango.
Naibu Meya huyo alisema jubilee ya hospitali hiyo inafika ikiwa imekuwa na historia ya kulea watoto yatima wengi wakiwemo ambao wazazi wao upande mmoja wapo lakini wamekimbia jukumu na hawataki hata kuwatembelea watoto hao hali ambayo alisema kuwa ni utatili mkubwa miongoni mwa watanzania .
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ambayo ni hatari katika kuiwezesha hospitali hiyo kumudu gharama za uendeshaji kwa kujitegemea baada ya wahisani kuanza kujiondoa taratibu alisema kuwa changizo la siku hiyo litasaidia kupata fedha kwa ajili ya ukarabati wa hospitali hiyo,uboreshaji wa kituo hicho cha kulea yatima na ununuzi wa vifaa bora vya kutolea tiba.
Aliwahamasisha wageni waliofika katika changizo hilo kwa kuwataka watoe michango yao na kuchana na dhana ya kudhani wahisani ndio wanaopaswa kuendesha hospitali hizo za misheni jambo a ambalo alisema kuwa ni hatari kubwa katika mfumo wa kujitegemea na kuondokana na fedha za aibu zenye masharti yasiyofaa zinazotolewa na wazungu.
Katibu wa Hospitali hiyo Japhet Kalindu akitoa utangulizi alisema kuwa hospitali hiyo ilianzisha na wamisionari wa kanisa Katoliki mwaka 1961 ambapo tangu hapo imekuwa ikitoa huduma bora bila ya kujali faida wakati wote.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo waliona ni vema kuwapo kwa changizo hilo litakaloisaidia kupata fedha zaidi ya miulioni 300 kwa ajili ya kukarabati hospitali ambapo alisema kuwa fedha hizo zitapatikana na kutoka kw awageni mbali wa ndani ya Wilaya wakiongozwa na mkuu wilaya ,wabunge,wafanyabishara na wadau mbali mbali wa hospitali hiyo.
Kalindu alisema lengo kubwa la fedha hizo ni kuwezesha Hospitali kuendelea kufanya kazi ya kutoa huduma ambazo ni sawa na bure kwa kiwango cha juu kulingana na uwezo wa wananchi wa eneo hilo.
Aliwashukuru wabunge ambao alisema kuwa kwa ujumla wao wametoa zaidi sh.milioni 1.4,mbunge Hilda Ngoye 400,000, Aliko Kibona mbunge wa Ileje sh.500,000. Mbunge Prof. David Mwakyusa sh.500,000 ,mkuu wa wilaya 250,000 na Mgeni rasmi akichangia sh.2,000,000, mfanyabiashara Richard Kasesera milioni 1,000,000 na kuungana na wachangiaji wengine kwa ajili ya kufanya jumla ya kiasi hicho kilichopatikana.
No comments:
Post a Comment