Monday, September 10, 2012

HANS POPE AZUNGUMZIA SUALA LA YONDANI KUTEKWA

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba mpango wa kumteka beki Kevin Yondan kama kweli ulikuwepo ni wa mtu binafsi na si maamuzi ya klabu, kwa sababu hawana sababu ya kumteka mchezaji wao halali kwa mujibu wa sheria zote.
“Yondan ni mchezaji halali wa Simba, kwa mujibu wa sheria zote, sasa tumteke ili iweje? Kama kweli hilo lipo, basi litakuwa la mtu binafsi na si mpango wa klabu. Na kama huyo mtu kafanya hivyo, hatuelewi kafanya hivyo kwa nia gani,”alisema Hans Poppe. Alisema baada ya kupata taarifa hizo, wanazifanyia kazi, watamuita huyo kiongozi anayedaiwa kuhusika na sakata hilo, ili wamhoji kujua nini ilikuwa dhamira yake.

“Jamani hakuna shaka yoyote Yondan ni mchezaji wa Simba, ameasi tu na sheria zitamrudisha Simba,”aliongeza Hans Poppe.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb alisema kwamba mchezaji wa zamani wa Simba, ambaye aliwahi kukutwa na kashfa ya kutaka kumhonga mchezaji wa timu pinzani akitumiwa na klabu yake hiyo, ndiye aliyemuingiza Yondan kwenye mtego.

“……..alikwenda kwa Yondan, akasema amekwenda kumsalimia na kwa kuwa wanafahamiana wamewahi kucheza wote wa Simba, Yondan hakuwa na tatizo. Baada ya mazungumzo akaaga anaondoka, akaomba asindikizwe hadi mjini, kufika mbele kidogo, yule mchezaji akaomba aendeshe gari la Yondan. Yondan akampa.

No comments:

Post a Comment