Tuesday, September 4, 2012

Tulikosea Wapi? Tufanyeje Kujirekebisha?

Hili ni jambo ambalo hunisumbua sana akilini mwangu, na ninaoma tulijadili kwa usikivu bila mipasho na ushabiki, ikiwezekana. Unaweza kuingia ofisini kwa mtu ukamkuta anaongea mambo ya kiumbea na rafiki yake kwenye simu wakismuliana jinsi mambo yalivyokuwa kwenye sherehe za harusi jana yake.

Unaweza kumsubiri pale labda kwa saa moja, na atakapomaliza hawezi hata kukuomba radhi, badala yake anaweza kukupa maneno ya mnyanyaso mengi sana.

Vile imekuwa ni jambo la kawaida sana tunapopatwa na majanga, serikali huwa inakuwa msitali wa mbele kuomba misaada kutoka nje, kama kuwa hawakuwa wamejiandaa kwa matukio ya aina hiyo.

Majanga mengi yamekuwa yanatokea nchini mwetu kila mara mara tena kwa pettern inayojiruidia rudia na wala hatujawa na mkakati wa kuyadhibiti. Siku hizi imekuwa ni kawaida sana mtu kutajirika haraka sana akishaingia kwenye madaraka ya kiserikali na kufungua akaunti kubwa sana kwenye nchi za nje, wakati ambapo tunaambiwa eti serikali haina pesa. Mambo ya aina hiyo na mengine yamenifanya kujiuliza kwa makini na kuhitimisha kuwa Tanzania:

(a) Hatujali kabisa ethics za kazi; nadhani hili linaeleweka sana.
(b) Hatujitumi kazini katika majukumu ambayo hayana rushwa; hatuogopi utendaji mbovu.
(c) Tunapowewa madaraka, tunaamini kuwa tuko entitled kuwa na madaraka hayo, na tunaweza kujipatia chochote kutokana na madaraka hayo.
(d) Tunathamini sana mali kuliko heshima; tuko tayari kulamba kiatu cha mwekezaji ili atupatie kitu kidogo.
(f) Tunapenda sana njia za mkato kwa kila kitu. Tukiwa na matatizo tunapenda kumtafuta mtu mwingine atutatulie
(g) Hatutaki kuwajibika wala kuwawajibisha tuliowapa majukumu. Kila wakati tunaamini kuwa tuko right, yanapotokea makosa katika mazingira yetu basi tunakuwa wa kwanza kutafuta mtu au kitu cha kulaumu; tukikosa kitu cha kulaumu basi tunamlaumu Mungu.



Mambo haya yameungana kiasi kuwa ni huwezi kuondoa moja ukaacha mengine. Kwa bahati mbaya mambo hayo ndiyo yanasoababisha tunashindwa kuendelea.

Kwa watu walioshi miaka ya sitini na ile ya sabini wakati bado kuna siasa za Ujamaa na Kujitegemea, mtakubaliana nami kuwa mambo hayo hayakuwamo miongoni mwa jamii yetu. Yalianza kukua kidogo kidogo mwanzoni mwa miaka ya themanini baada ya vita, na yakaua kwa kasi sana kuanzia mwishoni mwa miaka hiyo ya themanini, ambapo miaka ya leo hii tumefikia mahali ambapo ni alarming sana.

Nina maswali mawili ya kujiuliza:

(a) Ni wapi tulipokosea hadi tukajenga element mbovu hizo katika maisha yetu?

Nina imani hali ngumu ya uchumi iliyosababisha mapato halali ya wananchi kupungua vilisaidia kusababisha watu waanza kuachana na ethics za kazi kwa kutafuta rushwa, na kuanza kutumia nafasi za kazi zao kufanya biashara kinyume na masharti ya kazi. Lakini je kweli hiyo ndiyo iliyokuwa sababu pekee? Wizi wa mabilioni ya fedha za umma kweli ni kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi?

(b) Je tufanye nini sasa ili kurekebisha makosa hayo?

No comments:

Post a Comment