Rais wa UTPC Keneth Simbaya akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa tena |
Makamu wa Rais Jane Mihanji akijieleza kabla ya kuchaguliwa kwa kura za kishindo |
KENETH SIMBAYA amepitishwa tena kwa kishindo katika nafasi ya Rais wa Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) hiyo baada ya kupata kura 60 kati ya Jane Mihanji amepata kura za hapana 2 na kura za ndio 60 kati ya kura 62 zilizopigwa katika uchaguzi huo. Waandishi wa mtandao huu kutoka Dar es Salaam Esther Macha na Abdulaziz Video wanaripoti kuwaKatika uchaguzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam Simbaya amepata kuwashukuru wajumbe kwa ushirikiano mkubwa ambao amepata kuuonyesha katika kipindi kilichopita na hivyo kuwaomba ushirikiano huo uzidi katika kipindi kichacho. Simbaya amewataka wajumbe hao mkutano huo kuendelea kushikamana zaidi na kuwa katika uongozi wake uliopita amepata kuwa kiunganishi kizuri kati ya UTPC na wahisani kwa asilimia 150 na kuahidi kuendelea kufanya hivyo katika kipindi kijacho. Alisema kuwa ili kuweza kusonga mbele zaidi bado UTPC inahitaji viongozi wenye mahusiano mema na wahisani ili kuiwezesha UTPC kufanya vema zaidi. |
MWENYEKITI WA MBEYA PRESS KLABU CHRISTOPHER NYENYEMBE ACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA BODI YA UTPC
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe akiomba kura katika nafasi ya ujumbe wa bodi ambayo amepita kwa kura 33 kati ya 64 zilizopigwa |
No comments:
Post a Comment