Wednesday, September 5, 2012

Yatima watelekezwa Hospitali ya Igogwe Mbeya


WATOTO yatima waliopelekwa kulelewa katika kituo cha Hospitali ya Igogwe iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamebainika kuwa wametelekezwa na walezi na wazazi waliowapeleka katika kituo hicho.

Akielezea masikitiko yake kuhusu kutelekezwa kwa watoto hao, Naibu Meya wa Jiji la Mbeya  Chieffoda  Fungo alisema kuwa kitendo cha walezi na wazazi hao kufanya hivyo na kushindwa kutoa kutoa sh.5000 kwa mwezi   kwa ajili ya matunzo kunafanya kazi ya kuwatunza kuwa ngumu.

Kiongozi huyo alisema hayo  juzi wakati alipokuwa mgeni rasmi wa  changizo maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya maandalizi ya jubilee ya miaka  50 tangu kwa hospitali hiyo maalumu ya misheni ambapo zaidi ya sh milioni  20 zilipatikana ikiwa ni pamoja na ahadi.
Alisema  baada ya kutembelea  katika kituo hicho alisikia uchungu kupata taarifa  kuwa  wapo baadhi ya kinababa ambao walifiwa na wake zao na hivyo kutokana na kutokuwa na walezi wengine kuamua kuwapeleka  watoto hao katika kituo hicho  na kisha kukimbia majukumu kwa kushindwa hata kutoa sh.5000 kwa mwezi kiasi kilichopangwa na kama mchango.
Naibu Meya  huyo alisema  jubilee ya hospitali hiyo inafika ikiwa imekuwa na historia ya kulea  watoto yatima  wengi wakiwemo ambao wazazi wao upande mmoja wapo lakini wamekimbia jukumu na hawataki hata  kuwatembelea watoto hao hali ambayo alisema kuwa ni utatili mkubwa miongoni mwa watanzania .
Alisema  kuwa kutokana na hali hiyo ambayo ni hatari katika kuiwezesha hospitali hiyo kumudu gharama za uendeshaji  kwa kujitegemea baada ya wahisani kuanza kujiondoa taratibu alisema  kuwa changizo la siku hiyo litasaidia kupata fedha kwa ajili ya ukarabati wa hospitali hiyo,uboreshaji wa kituo hicho cha kulea  yatima na ununuzi wa vifaa bora vya kutolea  tiba.
Aliwahamasisha wageni waliofika katika changizo hilo  kwa kuwataka watoe michango yao na kuchana na dhana ya kudhani wahisani ndio wanaopaswa kuendesha hospitali hizo za misheni  jambo a ambalo alisema kuwa  ni hatari  kubwa  katika mfumo wa kujitegemea na kuondokana na fedha za aibu zenye masharti yasiyofaa  zinazotolewa na  wazungu.
Katibu wa Hospitali hiyo Japhet   Kalindu akitoa utangulizi alisema kuwa   hospitali hiyo ilianzisha na wamisionari wa kanisa Katoliki mwaka 1961 ambapo tangu hapo imekuwa ikitoa huduma bora bila  ya kujali faida  wakati wote.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo waliona  ni vema  kuwapo kwa changizo hilo  litakaloisaidia  kupata fedha zaidi ya miulioni 300 kwa ajili ya kukarabati hospitali  ambapo alisema kuwa fedha hizo zitapatikana na kutoka kw awageni mbali  wa ndani ya Wilaya wakiongozwa na mkuu  wilaya ,wabunge,wafanyabishara na wadau mbali mbali  wa hospitali hiyo.
Kalindu alisema lengo kubwa la  fedha hizo ni kuwezesha Hospitali kuendelea kufanya kazi ya kutoa huduma ambazo ni  sawa na bure kwa kiwango cha juu kulingana na uwezo wa  wananchi wa eneo hilo.
Aliwashukuru wabunge ambao  alisema kuwa kwa ujumla  wao wametoa zaidi  sh.milioni 1.4,mbunge Hilda Ngoye 400,000, Aliko Kibona  mbunge wa Ileje sh.500,000. Mbunge  Prof. David Mwakyusa  sh.500,000 ,mkuu wa wilaya 250,000 na Mgeni rasmi akichangia  sh.2,000,000, mfanyabiashara Richard Kasesera  milioni 1,000,000 na kuungana na wachangiaji wengine kwa ajili ya kufanya jumla ya kiasi hicho kilichopatikana.

No comments:

Post a Comment