Friday, August 31, 2012

WANAWAKE MBEYA WATAHADHARISHWA NA PEDI FEKI

  Hii bidhaa baadhi ya kina mama wameilalamkia haina ubora na inawatoa vidonda hatujapenda kutoa picha za akina mama hao walioleta ila zipo na kila mhusika tukimuuliza anasema watu wa viwango ndiyo wanahusika sasa mbeya hakuna ofisi za viwango je wafanyeje akina mama hao waliopata matatizo?

WANAWAKE mkoani Mbeya wanapaswa kujihadhari na bidhaa feki wanazotumia hasa za kujisitiri wakati wa siku zao (hedhi).

Uchunguzi uliofanywa na kuthibitishwa na baadhi ya wanawake umebaini bidhaa hizo feki zimekuwa zikiwavimbisha wanawake pindi wanapozitumia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema uwepo wa bidhaa zisizothibitishwa viwango vya ubora kwa kiasi kikubwa inachangiwa na kukosekana kwa ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Walibainisha kuwa hali hiyo imechangia bidhaa nyingi zinazoingia mkoani Mbeya kupitia mipaka ya Kasumulu kwa upande wa nchi ya Malawi na Tunduma kwa upande wa Tanzania kuwafikia walaji na watumiaji bila ya kukaguliwa ubora wake, hali ambayo ni hatari kwa afya zao.

Aidha, mmoja wa wamiliki wa viwanda vya kuzalisha mafuta ya alizeti kwenye soko la Sido eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya, Sophia Adamu, alisema hakuna ukaguzi wowote unaofanywa na TBS kwa mafuta yanayozalishwa kwenye viwanda vyao na kupelekwa moja kwa moja kwa walaji bila ya kuthibitishwa ubora wake na shirika hilo.

Alisema tangu ameanza kufanya biashara hiyo hajawahi kuwaona TBS wakienda kukagua bidhaa zao na kuthibitisa ubora na akashauri shirika hilo kufungua matawi mikoni hususan Mkoa wa Mbeya ambao una viwanda vingi vidogo vidogo.

No comments:

Post a Comment