Wednesday, September 12, 2012

CHADEMA CHAKIRI KUFADHILIWA NA WAHISANI TOKA NJE

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo.
 
 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema hayo jana katika semina iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa chama hicho na wageni kutoka shirika la Chama cha Kikristo cha Ujerumani (CDU) la Konrad Adenauer Stiftung (KAS). Kwa mujibu wa Dk Slaa, Chadema na KAS, wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa miaka sita sasa na ushirikiano huo umelenga zaidi kukuza demokrasia nchini. 
 
 
Dk Slaa alidai kuwa Chadema ni chama chenye uwazi kwa kila mtu na katika uhusiano wao na KAS, hakiletewi fedha moja kwa moja kwa ajili ya operesheni au maandamano, ila kujijenga kiuwezo. 
 
 
Pamoja na kusema kuwa KAS haitoi fedha moja kwa moja kwa Chadema kwa ajili ya maandamano na kampeni, lakini Dk Slaa alidai kuwa shirika hilo huwasaidia wastani wa Sh milioni 60 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho na kutoa elimu.
 
 Pia amesema kipo chama cha Uholanzi ambacho hakukitaja jina, lakini akakiri kuwa huwafadhili Sh milioni 20 kulingana na idadi ya wabunge walio bungeni. Pamoja na kusema kuwa ni kawaida kwa vyama vya mrengo mmoja kusaidiana duniani, Dk Slaa alisema chama hicho cha Uholanzi kinachowasaidia, pia hufadhili CCM fedha zaidi ya zinazopelekwa Chadema kutokana na chama hicho tawala kuwa na idadi kubwa ya wabunge.
 
 
Mbali na hilo Dk Slaa amedai kwamba kwa kuanzia wameamua kumshitaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Kwa mujibu wa madai ya Dk Slaa, tayari Chadema imefungua kesi namba 186 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Nape, ambaye anadaiwa alitamka Chadema kufadhiliwa kutoka nje. Dk Slaa amedai kuwa kesi hiyo itakapokuwa ikiendelea, wataongeza watu wengine walioeneza kauli hiyo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema ili uchumi uwe endelevu, lazima wananchi wapewe haki na kuruhusu sekta binafsi kusimamia uchumi na si rahisi kusimamia uchumi kwa sera za kijamaa.
CHANZO: HABARILEO

Monday, September 10, 2012

M4C YA CHADEMA, YAWALETA CUF NA MCHAKAMCHAKA MPAKA 2015, KAZI IPO KWA CHAMA CHA MAPINDUZIWA

Wafuasi wa Chadema, Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam Jumapili

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SABA WA WALIMU WA AFRIKA (African Confederation for Principles ACP) JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga walimu kutoka nchi za  Afrika wanaohudhuria mkutano wa 7  wa ACP, unaojadili kuhusu maboresho ya Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo na Mheshimiwa Makamu wa Rais na unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika hususani zile zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia walimu wakati akifungua mkutano wa siku 3 kwa walimu wa nchi za Afrika unaojadili kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika zinazotumia lugha ya Kingereza katika ufundishaji.
 Baadhi ya wawakilishi wa walimu waliohudhuria mkutano huo kutoka nchi za Afrika leo katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Mwakilishi wa Walimu kutoka Uganda, akitoa neno la shukrani.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akitembelea mabanda ya maonyesho katika mkutano huo.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya S. Scientific Centre, ambao ni wasamabazaji wa vitabu vya mashuleni, Shana William, wakati akitembelea mabanda ya maonyesho katika mkutano huo, leo.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisoma kitabu katika moja na banda la maonysho katika mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wawakilishi wa walimu kutoka Kenya waliohudhuria mkutano wa siku 3 wa walimu wa nchi za Afrika kuhusu kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika.
 Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Uganda.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na walimu baada ya kumaliza kufungua rasmi mkutano huo.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAIPIGA TAFU KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga akipokea msaada wa fulana 1000 za kuhamasisha wiki ya usalama barabarani na vipeperushi 500 kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye makao makuu ya Trafic jijini Dar es salaam, kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti Nandi Mwiyombela.
Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 17.5 na kampuni hiyo imesema inaangalia uwezekano wa kuchapisha vipeperushi vingine kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam ambapo hivi vya awali vitapelekwa mikoani
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga akipokea msaada wa vipeperushi 500 kwa ajili ya kuhamasisha wiki ya usalama barabarani kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika mkwenye makao makuu ya Trafic jijini Dar es salaam, kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti Nandi Mwiyombela.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpingaakizungumza katika makabidhiano hayo wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wanaofuatia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mpunda na Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti Nandi Mwiyombela.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mpunda  akizungumza katika makabidhiano hayo kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti Nandi Mwiyombela.

Minister for Foreign Affairs and International Co-operation,Bernard Membe talks to Wananchi on Lake Nyasa border dispute

Beautiful view of Lake Nyasa in Mbamba Bay Ward.
 Hon. Bernard K. Membe (MP), Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, washes his hands with Lake Nyasa water in Mbamba Bay Ward area, in Ruvuma Region.
Hon. Membe greets one of the residents living in Mbamba Bay, offshore Lake Nyasa. 
 Hon. Membe talks to the young generations, assure them of peace, security and tranquility in their lives. 
 Hon. Bernard K. Membe (MP), Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, holding a book containing one of the earlier maps, indicating the borderline on Lake Nyasa lies in the median line. 
 Hon. Membe speaks with elders in Liuli Ward, during his two-day tour mission in Ruvuma Region.  Liuli Ward is also located in the area of Lake Nyasa.  Others in the photo are Capt. John Damiano Komba (MP - Mbinga West) (1st left), the Ruvuma Regional Commissioner, Hon. Said Mwambungu(2nd left), Mr. John M. Haule (1st right), Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation and Mr. Ernest Kahindi (2nd right), District Commissioner of New Nyasa District.
Hon. Bernard K. Membe (MP) talks to Wananchi of Mbamba Bay Ward in Ruvuma Region
 One of the elders, who was a policeman during the colonial era, expressing his sentiments about the Lake Nyasa border dispute.
 Mr. Ndembeka (above) is a fourth generation after the Germany rule and descendant of the first councilor of Tanganyika origin. Behind is Ambassador Irene Kasyanju, Director for Legal Affairs in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 
One of the Wananchi in Songea District, expresses her sentiment over the Lake Nyasa border dispute.
 Hon. Membe listens to various sentiments from Wananchi of Songea District on Lake Nyasa border dispute.  Others in the photo include Ruvuma Regional Commissioner Hon. Mwambungu (left to Hon. Membe), Songea District Commissioner and  Capt. John Kombo, (MP- Mbinga West) (2nd left) and Mrs. Membe (3rd left), who originates from Mbamba Bay Ward. 
 Liuli Ward elders listening to Hon. Membe.
Some of the Mbamba Bay elders.  Others in the photo includes Ambassador Irene Kasyanju (1st left on 2nd line), Director for Legal Affairs in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operatio, Ambassador Dr. Mohammed Maundi (2nd left on 2nd line), Director for Mozambique-Tanzania Centre for Foreign Relations, Mr. John M. Haule, Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation and Mr. Assah Mwambene (standing behind Amb. Kasyanju), Director of Information and Government Spokesperson, Ministry of Information, Culture, Youth and Sports.All Photos by Tagie Daisy Mwakawago and Mr. Assah Mwambene
-----

By TAGIE DAISY MWAKAWAGO

A Government delegation led by the Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, Hon. Bernard K. Membe (MP) was in Ruvuma Region for a two-day mission aimed at briefing the locals in the Lake Nyasa area on the ongoing negotiations over the border dispute with Malawi.
The delegation that also included members of the Tanzania People’s Defense Forces (TPDF), the President’s Office, the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development and the Ministry of Information, Culture, Youth and Sports visited and talked to Wananchi in Mbamba Bay, Liuli, Lituhi Wards in the New Nyasa District and Songea District.
On arrival at Ruiko Airport in Songea yesterday, the delegation was received by the Ruvuma Regional Commissioner, Hon. Said Mwambungu and other senior regional officials.  Hon. Membe thanked the Regional Commissioner for the warm reception and hospitality accorded to himself and his delegation. 
Introducing members of his delegations, the Minister said “we are here for two objectives, brief the Wananchi on the ongoing bilateral talks, get the oral tradition and local knowledge from elders around Lake Nyasa,” assuring Wananchi security and normalcy in their daily activities. 
Tanzania and Malawi have been in border dispute over the Lake Nyasa since the attainment of each country’s independence.  Malawi claims right to the whole Lake Nyasa, while Tanzania claims ownership to half of the Lake.
“We stand firm that the border runs in the middle of the Lake and that even if we go to the International Court of Justice (ICJ), we will be ready to justify that,” said the Minister. 
The Minister said that the Government has been working diligently on resolving the dispute diplomatically, and if all other efforts fail, then the ICJ will likely be the final course to take.     
The mission started in Mbamba Bay Ward, where the Minister spoke with the elders.  One of them was Mr. Gideon Liganga Ndembeka (85), who articulated a detailed history of Lake Nyasa, stating that the frontier or borderline of the two countries was and still is in the middle of the Lake. 
He demonstrated that fact with the help of historical books written by the British Colonial Government, whereby the frontier between Tanzania and Malawi was located in the middle.  Mr. Ndembeka provided the said books to Hon. Membe, to assist the Government in building its case. 
Moreover, one of the prominent fishermen in Mbamba Bay strongly raised an observation of the fact that the frontier is in the middle and not otherwise.  This is supported by regular practice of Ship Captains of either side who observe the change of flag rule, when entering each others’ waters.

“This change of flags always takes place at the median point of the Lake Nyasa where the water demarcates itself in a form of a ridge or edge shape,” he said, adding that they usually call it an upper point. 

This point was supported by other elders, who asserted that when entering the Tanzanian waters at the upper point, Malawian ships will lower and replace their flags with Tanzania flags, an exercise which Tanzanian ships do when entering Malawian waters at the upper point.   
On his visit to Liuli Ward, Hon. Membe met with various elders aging between 60 to 98 years of age, who most of them expressed their agony over the Lake Nyasa border dispute.  One of them, Ms. Mariam Chiundu said “this is not a man-made Lake, and therefore one cannot claim sovereignty over it.   It is a natural feature from God, and it ought to be shared.”  Her argument was centered at the fact that God is not discriminative.
During the mission, Hon. Membe also stopped by Lituhi Ward and Songea District where the sentiments were overwhelmingly similar to those expressed in other visited Wards.  However, in Lituhi, the elders unanimously said that River Songwe naturally demarcates the River into two halves, and all the way to the Shire River towards the Mozambique side.  This observation supports the claim provided by the elders in Liuli and Mbamba Bay Wards that the upper point marks the median line of the Lake between the two countries.
For Songea District, where the two-day tour ended, the Minister was told about the school, church, cemeteries, farm yards and a village which were all submerged in the Lake as a result of drifting and expansion of the water mass towards the land. To their dismay, that would mean that if the border was set in the shore at 1890 where could it be today? 
In his closing statement, Hon. Membe assured the Wananchi of Songea District, and all who are living around the Lake Nyasa area, of their security and properties, and that the Government wants them to continue with their daily activities without any worries.

HANS POPE AZUNGUMZIA SUALA LA YONDANI KUTEKWA

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba mpango wa kumteka beki Kevin Yondan kama kweli ulikuwepo ni wa mtu binafsi na si maamuzi ya klabu, kwa sababu hawana sababu ya kumteka mchezaji wao halali kwa mujibu wa sheria zote.
“Yondan ni mchezaji halali wa Simba, kwa mujibu wa sheria zote, sasa tumteke ili iweje? Kama kweli hilo lipo, basi litakuwa la mtu binafsi na si mpango wa klabu. Na kama huyo mtu kafanya hivyo, hatuelewi kafanya hivyo kwa nia gani,”alisema Hans Poppe. Alisema baada ya kupata taarifa hizo, wanazifanyia kazi, watamuita huyo kiongozi anayedaiwa kuhusika na sakata hilo, ili wamhoji kujua nini ilikuwa dhamira yake.

“Jamani hakuna shaka yoyote Yondan ni mchezaji wa Simba, ameasi tu na sheria zitamrudisha Simba,”aliongeza Hans Poppe.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb alisema kwamba mchezaji wa zamani wa Simba, ambaye aliwahi kukutwa na kashfa ya kutaka kumhonga mchezaji wa timu pinzani akitumiwa na klabu yake hiyo, ndiye aliyemuingiza Yondan kwenye mtego.

“……..alikwenda kwa Yondan, akasema amekwenda kumsalimia na kwa kuwa wanafahamiana wamewahi kucheza wote wa Simba, Yondan hakuwa na tatizo. Baada ya mazungumzo akaaga anaondoka, akaomba asindikizwe hadi mjini, kufika mbele kidogo, yule mchezaji akaomba aendeshe gari la Yondan. Yondan akampa.

Poleni waandishi na Polisi, Hongereni wanasiasa, nakugomea Dr, Slaa

NASHINDWA kuyazuia machozi yangu yanapobubujika na kudondoa kwenye kope za macho yangu hasa ninapokumbuka kifo cha Mwandishi Daud Mwangosi na watanzania wengine waliokufa na kujeruhiwa kwenye mikutano ya kisiasa hapa nchini kwetu Tanzania.

Nianze kwa kutoa pole kwa wananchi wote wakiwemo wanataaluma wote wakiwemo waandishi wa habari na askari Polisi Tanzania walioumia na wanaotarajiwa kuumizwa katika mikutano ya wanasiasa wetu kupitia ‘’Chama cha Migomo na matatizo yasiyokwisha’’ huku Polisi wakikosa mtu wa kuwasemea na kuendelea kuumizwa na kutukanwa majukwaani.

Sitaki kuorodhesha orodha ndefu ya matukiom ya kisiasa yaliyowahi kutusikitisha wengi hasa wananchi na askari polisi wanapoumizwa na hata vifo kutokea kutokana na ukaidi wa wanasiasa wenye uchu wa madaraka hapa nchini.

Nawapa ‘’Hongera’’ sana wanasiasa mnaaona ni fahari mioyoni mwenu kuona damu za watanzania zinamwagika na wengine wakipa ulemavu katika mikutano yenu ili tu ninyi mpate nafasi ya upangaji  pale Ikulu. Hongereni sana lakini mjue kuwa damu hizo zitakuwa juu yenu na watoto wenu.



Kama nilivyoshindwa kujizuia kutokwa na machozi vivyo hivyo nakosa kujizuia kuwaza vifo na majeraha vinavyotokea kwenye mikutano ya wanasiasa kuwa si kafara.

Naomba usilie msomaji wangu, futa machozi hata kama wewe unajua jambo hili kwa undani zaidi kikubwa utambue kuwa maisha ni safari ndefu isiyokuwa na likizo.

Kutoka hapa Nyikani naleta matumaini mapya kwenu  na kwa pamoja tukumbuke kuimba wimbo wetu wa kuwasha mwenge huku tukikumbuka maneno aliyoyatamka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Baadhi ya maneno ambayo aliyatamka Mwalimu Nyerere alisema kuwa Sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka Mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu na ulete Tumaini.

Pale ambapo hapana matumaini, Upendo mahala ambapo pana chuki, Heshima ambapo pamejaa dharau.

Uhalisia wa maneno hayo ya Mwalimu wakati wa kuwasha Mwenge wa uhuru mwaka 1962 sasa unaonekana ambapo kwa sasa bila kutafuna maneno ni kwamba dharau zimezidi kwa watawala wetu na watu wanaoongoza dharau hizo ni wale ambao kila kukicha wanapaza sauti kuwa Mwenge ufutwe.

Wanapiga kelele na kupaza sauti zao ili kuendeleza dharau zao katika jamii na wanajua kuwa Mwenge unawakosesha amani mioyoni mwao na kushindwa kuendeleza dharau kwa watawala waliopo madarakani huku Mwenge ukipita kila kona na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na wananchi wakati wao wanasema kuwa katika nchi hii hakuna kinachofanyika ‘’wao wanawaza maandamano tu’’

Mwenge ambao unaleta matumaini kwa wale waliokata tamaa na kujua propaganda za kuwafinyanga fikra zao ili waamini kuwa Serikali haifanyi lolote, umekuwa sumu kwao maana hata Viongozi au wakimbiza Mwenge wameendelea kukemea utengano wa kikabila, Rangi na uasi wa aina yeyote katika nchi yetu na huo umekuwa mwiba kwao.

Mfano mzuri wa wtu hao ambao mimi binafsi na baadhi ya waandishi wa habari nchini Tanzania tumetangaza rasmi kugoma kuandika habari zinazomuhusu Dr. Wilbroad Slaa kutokana na kutoridhishwa na mambo yake.

Kwa muda mrefu Dr. Slaa amekuwa chanzo cha mambo mengi hasa ya kutotii sheria bila shuruti na kwa kuonesha kile anachokiamini kuwa yeye ndiye yeye katika nchi hii ameamua na kujiridhisha kuwa anaweza kuwashika masikio hata waandishi wa habari kwa kufanya lolote hata kuingilia taaluma yao.

Nakumbuka Tarehe 4.09.2012 pale katika Kijiji cha Busoka kata ya Itete wilaya ya Rungwe (Tukuyu) mkoani Mbeya wakati wa Mazishi ya Mwandishi Daud Mwangosi ambapo Dr. Slaa aliamua kujivika umwamba na kujifanya yeye ni zaidi ya waandishi wa habari.

Katika mazishi ya Mwangosi Kaimu Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa Mpiganaji Francis Godwin alisema kuwa tangu mwili wa Mwangosi ukiwa Iringa alipobaini kuwa Chadema ‘’walifurahia’’ kuuawa Mwangosi, walitaka kiuubeba mwili wa marehemu na kuhodhi msiba huo, aliaqmua kutangaza kuwa Msiba huo si wamwanasiasa bali ni wa-Mwandishi wa habari jambo ambalo liliwaudhi sana Chadema.

Mpiganaji mwenzangu Francis Godwin ambaye watu wengi wananichanganya naye mimi Gordon Kalulunga, alipofika na mwili wa marehemu Tukuyu aliwatangazia tena wananchi kuwa msiba huo haukuwa wa wanasiasa.

Baada ya kuona Francis anaendelea kukomelea msumari huo wa moto kwa wanasiasa akiwemo Dr. Slaa, Chadema hawakuridhika maana walijua kuwa kifo na maiti ya mwangosi ni moja ya vitega uchumu vya siasa zao kama walivyozoea.

Dr. Slaa alipoinuka akasema kuwa mwandishi huyo ingawa hakumtaja jina, alidai kuwa hajui alitendalo na amemsamehe kwasababu yeye binafsi alikuwa na mahusiano mema na Mwangosi tangu akiwa Mbunge na mambo mengine ambayo hakuweza kuyataja.

Ni utovu wa nidhamu kwa mwanasiasa kama Dr. Slaa anayehisi kuwa anaheshimiwa halafu yeye akiwa hataki kujiheshimu.

Prof. Mark Mwandosya alikomelea msumariu katika mazishi hayo na kutamka wazi kuwa ni upuuzi kujitafutia umaarufu katika matatizo ya watu hasa msiba.

Labda mimi na wenzangu nitamke rasmi kuwa natoa tamko la kutokuwa na imani na Dr. Slaa na ninasusia kuandika habari zake kutokana na dharau zake kwa waandishi wa habari huku akiamini kuwa yeye ni mungu mtu anayeweza kunye4nyekewa na kila mtu. Ni upuuzi mkubwa.

Sitoi msimamo huo kwasababu Mwangosi ni kabila langu la watu ambao ni wenye msimamo duniani bali natoa tamko hili kwa kuwa Chadema naamini kuwa ni chanzo cha kifo cha Mwangosi na kutotii sheria bila shuruti kwa wanasiasa wa Chadema hivyo fikra zangu ambazo naamini ni sahihi zinatamka kwa herufi kubwa kuwa kwasababu wameona kifo cha Mwangosi ni mtaji wa kisiasa kwao sina imani nao.

Katika makala haya kama ilivyo kawaida ya wahuni wachache natarajia kupata matusi kupitia sms na vitisho huku wakisaqhau kuwa siku za kuishi kwangu anazijua zaidi Mungu aliyerumruhusu Mama yangu mzazi kuzaliwa kwangu.

Msipate shida kufikiri zaidi juu ya uhai wangu maana naamini ukweli huu utadumu zaidi kuliko uhai nilio nao, na ninamalizia kwa kusema kuwa waandishi wa habariu hata kama tumeahidiwa kuwa tutakuwa wapiga picha wa Rais wa kufikirika ajaye, tutambue kuwa atakayekuchoma kwa kalamu akiingia madarakani atakuchoma kwa risasi kama hivi atumiavyo Dr. Slaa kutu,ia vyombo vya habari kuikuza Chadema, namaliza kwa kusema Poleni waandishi na Polisi, Hongereni wanasiasa, nakugomea Dr, Slaa.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu 0754 440749

WAANDISHI WAMENANGWA NA TUNDU LISU, TUSUBIRI TAMKO


Na Hamis Shimye
TAALUMA ya uandishi wa habari nchini kila kukicha imeendelea kudharauliwa na wanasiasa na baadhi ya viongozi ambao wanajiona taaluma zao ndio bora na zenye uwezo wa kuhoji na kuakisi mambo.

Mfumo huo umeendelea kuota mizizi huku hata zile klabu, majukwaa na mabaraza ya uandishi wa habari yakiwa kimya na badala yake kuzungumzia mambo mengine ambayo hayana faida kwa mwandishi wa habari.

Uandishi wa habari Tanzania unakumbukana na changamoto lukuki ambazo zilipaswa kuwa sehemu ya mjadala kwa vyama vilivyopewa dhamana ya kuwaongoza waandishi wa habari ambao maisha na mfumo wa kazi zao umekuwa kama mchezo wa bahati nasibu.

Kitendo ambacho kinafanya thamani na hadhi ya mwandishi kila kukicha kupotea huku majina ya dharau nayo yakizidi mara 'watu wamshiko', 'makanjanja' au 'vihiyo'. Yote haya yanasababishwa na ubinafsi  na ukasuku wa kukariri matamko.

Kauli ya kashfa na Mbunge Tundu Lissu (Singida Mashariki - CHADEMA) kuhusiana na wajumbe wa tume walioteuliwa na serikali kuhusiana na kifo cha Mwandishi wa habari Daud Mwangosi kuwa baadhi yao hawana uwezo ni fedheha kubwa kwa wajumbe hao na tasnia nzima.

Mbunge huyo aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa chama chake kutokuwa na imani na tume hiyo hasa kutokana na kuwa na wajumbe baadhi aliodai wasiokuwa na ueledi wa mambo wanaochunguza.

Katika mkutano huo, Lissu alizungumza mambo mengi juu ya tume hiyo, lengo likiwa kuaminisha umma kuwa tume hiyo haifai na ndiyo maana chama chao wanaikataa huku akitaja majina ya wajumbe wa tume hiyo ambayo kimtazamo wake yeye anasema hawana uwezo.

Hata hivyo, muktadha wa hoja hii hautakuwa kuzungumzia uwezo wa kila mjumbe ndani ya tume hiyo, bali ni udhaifu wa vyama vyetu ambavyo navyo vinapotezwa katika mlengo wa kusimamia maslahi ya waandishi na kuanza kuwa watoa sauti ya wanasiasa kushindana kuikataa tume.

Kuchaguliwa kwa Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Stephen Ihema na wajumbe wengine wakiwemo mahiri katika tasnia ya habari kama Theopil Makunga (Jukwaa la Wahariri) na Pili Mtambalike (Baraza la Habari Tanzania) ilikuwa ni sehemu ya waandishi na klabu za habari kufurahia na kuipongeza serikali.

Kufurahia huko kunatokana na kifo cha Mwangosi ambaye ni mwenzetu kuwa kinachunguzwa na waandishi wenyewe, hivyo kutolewa kwa kauli za dharau kuwa waandishi wa habari hawawezi kuchunguza kifo ni tusi kubwa ambalo lilipaswa kukemewa na si kuachwa kama inavyotaka kufanywa.

Nakumbuka katika jali ya MV Bukoba, mmoja wa wana habari mahiri nchini Jenerali Ulimwengu alikuwa mjumbe wa tume iliyochunguza chanzo cha ajali hiyo. Mbona mambo yalikwenda sawa au kwa kuwa Lissu alikuwa hajapata umaarufu?

Japokuwa katika suala zima kuhusiana na tukio hilo waandishi walitofautiana kimtazamo na kifikra, lakini linapokuja suala la kudharauliwa, tunapaswa kuwa pamoja na kukemea. Kinyume chake baada ya kunang'wa na Lissu tunatakuja kupewa tusi kubwa zaidi.

Mwenye uwezo na ueledi wa kuchunguza kifo si mwanasheria pekee? Lisu anapaswa kutambua hilo na kuachana na mawazo ya Mfalme Jua,  juu ya kile anachokiamini kuwa ni sahihi na hapaswi kupingwa au kukatazwa na mtu.

Jamii inaelimishwa na kufundishwa kupitia mifumo tofauti ya maisha na ndiyo maana wanasaikolojia wanaamini tabia ya mtu ni rahisi kuifahamu kupitia matamshi na matendo yake kuwa ni makuzi gani aliyapata utotoni.

Sitaki niamini kuwa klabu, jukwaa na hata baraza lenyewe halijasikia maneno ya kejeli ya Lissu, bali naamini yapo makundi ndani ya waandishi wa habari likiwemo la wale walio tayari kwa lolote ili mradi wawanufaishe wengine na hasa wanasiasa au watwana wao.

Hilo litapongezwa kwa matamko au hata kwa kujitokeza na kusukuma magari yao kuwa hawa kwa mtazamo wao kuwa hao ni mashujaa na wazalendo wa nchi hii .

Hivyo, ningetamani nguvu iliyotumika kutoa tamko la kuwataka polisi wakae meza moja na CHADEMA kumaliza tatizo, ingetumika kutoa tamko juu ya dharau ya Lissu na chama chake kwa waandishi wa habari nchini.

Mchina Mbaroni Kwa Kuchimba Madini Kwenye Pori La Akiba.


Mtambo wa kuchimbia madini ambao Raia wa China walikamatwa wakiutumia katika pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkansi kinyume cha sheria.Raia huyu wa china amehukumiwa kulipa faini na kuamriwa kuondoa mtambo huo katika pori hilo.

Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.

 Na:  Veronica Kazimoto – MAELEZO
 Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba  madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya,  mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine  aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu  cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.

Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.

Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi  kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba. Aidha  Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.

Chaoxian Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai 25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa huru.

Saturday, September 8, 2012

KENETH SIMBAYA AULA TENA UTPC JANE MIHANJI AWA MAKAMU WAKE


Rais wa UTPC Keneth Simbaya akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa tena

Makamu wa Rais Jane Mihanji akijieleza kabla ya kuchaguliwa kwa kura za kishindo






KENETH SIMBAYA amepitishwa tena kwa kishindo katika nafasi ya Rais wa Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) hiyo baada ya kupata kura 60 kati ya Jane Mihanji amepata kura za hapana 2 na kura za ndio 60 kati ya kura 62 zilizopigwa katika uchaguzi huo.

Waandishi wa mtandao huu kutoka Dar es Salaam Esther Macha na Abdulaziz Video wanaripoti kuwaKatika uchaguzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam  Simbaya amepata kuwashukuru wajumbe kwa ushirikiano mkubwa ambao amepata kuuonyesha katika kipindi kilichopita na hivyo kuwaomba ushirikiano huo uzidi katika kipindi kichacho.

Simbaya amewataka wajumbe hao mkutano huo kuendelea kushikamana zaidi na kuwa katika uongozi wake uliopita amepata kuwa kiunganishi kizuri kati ya UTPC na wahisani kwa asilimia 150 na kuahidi kuendelea kufanya hivyo katika kipindi kijacho.

Alisema kuwa ili kuweza kusonga mbele zaidi bado UTPC inahitaji viongozi wenye mahusiano mema na wahisani ili kuiwezesha UTPC kufanya vema zaidi.

MWENYEKITI WA MBEYA PRESS KLABU CHRISTOPHER NYENYEMBE ACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA BODI YA UTPC


Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe akiomba kura katika nafasi ya ujumbe wa bodi ambayo amepita kwa kura 33 kati ya 64 zilizopigwa

Bodi Ya Mikopo Yatafuna Fedha Za Wanafunzi

 Financial statement inayoonyesha kiwango anachodaiwa wakati fedha hizo hazikulipwa na mwanafunzi huyu bado anadaiwa na chuo na kimeshikilia vyeti vyake
 Barua ambayo chuo kiliandika kuonyesha kuwa fedha zilirudishwa bodi baada ya kuwa hazikusainiwa na wanafunzi.na kuwa fedha ya mwaka wa pili haikulipwa kabisa na bodi ya mikopo
 Baada ya kufuatilia suala lake,alilifikisha hadi wizara ya elimu,na wizara ikawaandikia bodi kutaka kujua ukweli wa madai haya,Barua hii haikujibiwa
Baada ya bodi kutojibu barua ya kwanza,wizara iliandika tena kuulizia suala hilo,Hadi sasa bado bodi haijajibu kitu.

Bodi ya mikopo,inalalamikiwa kutafuna fedha za mwanafunzi MWESIGA CHRISTIAN MICHAEL aliyehititimu DUCE mwaka 2011.
 
Bodi inaonekana hawakulipa ada yake ya mwaka wa kwanza na wa pili,bali walilipa ya mwaka wa tatu pekee.
 
Alipokuwa akifuatilia akiwa bado chuoni alikuwa akiambiwa hakuna tatizo na ada zote zitalipwa.
 
Bali amejikuta akidaiwa na chuo ada ya miaka 2 zaidi ya milion 2 na chuo kimezuia vyeti vyake.Bodi ya mikopo ambayo aliingia nayo mkataba sasa inasema haimtambui na bajeti yake haipo tena.
 
Hata hivyo uchunguzi umegundua kuna udanganyifu kwa upande wa bodi kwani financial statement waliyotoa inaonyesha amelipiwa ada.
 
Isipokuwa mjengwablog,imegundua kuwa bodi,ama watumishi wake walighushi kwa makusudi na kubadili majina ya mnufaika na kulipa mtu hewa kwa miaka 2,ila wakalipa mtu stahiki mwaka wa tatu pekee.Ajabu hata hivyo,Mwesiga Christian Michael,hakunufaika na fedha hizo,bado anadaiwa na chuo na vyeti vyake vimezuiwa.Ajabu ni kuwa inaonekana anadaiwa zaidi ya milioni 7 wakati hazikulipwa fedha hizo.
 
  Ni wazi kuna udanganyifu na au wizi kwenye bodi ya mikopo,na mjengwablog imeshindwa kujua ni vipi bodi imekaidi kujibu barua za wizara mara mbili juu ya madai ya Mwesiga.

Tunadhani wenye kuhusika watafutwe na mamlaka husika ili wawajibike kwa wizi walioutenda.Hadi sasa Mwesiga hajapata ajira kwa sababu hana vyeti vya shahada.