Monday, September 3, 2012

Taswira Za Mkutano Wa Wabunge Wa Afrika Mashariki Na Waandishi Wa Habari Jijini Dar es Salaam

 Mbunge  wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Tasilimu akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki  ambao wataufanyia kazi katika kikao cha  Bunge kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam.
  Mbunge  wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Angela Kiziga  ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu  tofauti ya kiuchumi na maendeleo baina ya nchi tano wanachama wa jumuia hiyo .
 Katibu  wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji (kulia) akiongea jambo na  Abdullah Mwinyi (kushoto) ambaye ni Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge hilo wakati wa mkutano baina yao na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya
Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kuviomba  vyombo vyao viweze kutambulisha timu ya wabunge hao tisa kwa watanzania ili wapate kuwafahamu kama wawakilishi wao wanaosimamia masuala ya taifa. Kulia ni Mbunge Angela Kiziga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira katika bunge hilo.Picha na Habari Maelezo

No comments:

Post a Comment