Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi wa SUMATRA Huduma za Uzidhibiti wa Bandari na Usafiri Majini Ndugu Peter Lupatu ambaye yupo Mkoani Rukwa kwa ajili ya ukaguzi wa bandari ya Kasanga na vifaa vya usafiri wa majini katika ziwa Tanganyika ikiwemo meli ya Mv Liemba na Mv Mwongozo. Mkuu huyo Mkoa alimuomba Mkurugenzi huyo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya majini hususani Meli ili kuepusha ajali mbaya zinaweza kujitokeza kama ilivyotokea kwa meli za Mv Spice Islanders na Mv Skagit katika bahari ya Hindi. Alisema ajali nyingi husababishwa na ubovu wa vyombo hivyo ambavyo vinahitaji ukarabati wa mara kawa mara.

Mkoa wa Rukwa unapakana kwa karibu sana na Nchi za Kidemeokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia ambapo mpaka wa nchi hizo upo katika ziwa Tanganyika. Kwa kuona umuhimu wa kuziunganisha nchi hizo kibiashara Serikali imeamua kujenga bandari ya Kasanga ambayo itakuwa kiunganishi kikubwa cha kibiashara na nchi hizo. Sio bandari peke yake bali pia barabara za lami kutoka Mkoa wa Mbeya (Tunduma)-Sumbawanga hadi Kasanga ilipo bandari hiyo inaendelea kujengwa na inategemewa kukamilika mwakani 2013. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment