Monday, September 3, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI..........UONGOZI WA BLOGU YA KALULUNGA UNATOA POLE NA USHAURI KUFUATIA KIFO CHA MWANDISHI WA IRINGA


 KAMANDA MKUU WA KIKOSI KAZI CHA MTANDAO WA www.kalulunga.blogspot.com GORDON KALULUNGA
POLISI WAKIWA WAMEMSHIKILIA MWANDISHI DAUD MWANGOSI KABLA YA MAUTI HAYAJAMPATA.

UONGOZI wa Mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com unaungana na wanadamu wengine popote duniani kutoa pole kwa familia ya aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Chanel Ten Daud Mwangosi aliyefariki jana katika sintofahamu ya kutoelewana na kutokea fujo kati ya wananchi wanakipenda chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Iringa nchini Tanzania na Jeshi la Polisi.

Sisi tukiwa wanahabari nchini Tanzania na kumiliki mtandao huu, tumesikitishwa sana na kifo cha mwanataaluma mwenzetu ambaye pia alikuwa kiongozi wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa.

Pamoja na masikitiko yetu, tunatamka kuwa ni muhimu Serikali ikatoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji wake pamoja na watu wanaofanya kazi nao yaani Raia kutii sheria bila shuruti, wanataaluma kuzingatia sheria za kazi zao na watendaji wa Serikali kutumia criticle thinking.

WANANCHI.
Kwa upande wa wananchi, kuwepo elimu madhubuti ya kutii sheria bila shuruti ambapo sisi kama kikosi kazi cha mtandao wa kalulunga.blogspot.com, tunaamini kuwa elimu ya namna hii ingekuwepo kwa uhalisia wake vurugu za jana mkoani Iringa zisingetokea kwasababu viongozi wa chama hicho cha siasa wangeweza kuwazuia wenyewe wafuasi wao, lakini kwasababu wananchi ikiwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa hawataki kuikubali elimu hiyo iliyowajia ukubwani ndiyo maana yakatokea hayo yaliyotokea na kutusikitisha sana.

WAANDISHI WA HABARI.
Wito wetu  kwa waandishi sote, ufike wakati kutodharau sheria zinazotuongoza kwasababu si kila Polisi au mfanyakazi wa Serikali anayetufahamu hata kama tunaenda kuuliza vitu vya Msingi, hivyo nashauri katika mikusanyiko ya mikutano ni muhimu kuvaa vitambulisho vyetu vya kitaaluma hata kama tunaupenzi/uanachama na uongozi katika vyama vya siasa.

POLISI.
Kwa upande wa Jeshi la Polisi Serikali iweze kuwafundisha somo la kufikiri kwa kina na kujenga hoja yaani Criticle thinking (sisi kama kalulungablogu) tutafundisha mkihiyaji kwa gharama kidogo, somo ambalo litaweza kuwasaidia sana katika kutimiza majukumu yao kwa mfano tunaamini kuwa askari hao wangekuwa na elimu hiyo kikamilifu wakati wamemkamata Mwangosi au alipokuwa akiwaendea bila silaha yeyote na kuhoji ilikuwa ni kiashiria kujua kuwa huyu ni mtu ambaye si adui.

Asanteni sana na huu ndiyo msimamo wetu.

No comments:

Post a Comment