Friday, August 31, 2012

WANAFUNZI NA WAAJILIWA WENGI WANATUMIA VYETI VISIVYO VYAO.

* 264 Walifanya mtihani kidato cha sita Februari 2009 kwa kutumia sifa zilizowahi kutumiwa miaka iliyopita.

* 160 sifa za vyeti vyao zilitumiwa kujisajili na wanachuo wa ualimu daraja A na stashahada ya ualimu mei 2009.



WANAFUNZI wengi nchini hasa wa shule za Sekondari, vyuo na waajiliwa katika nafasi mbalimbali Serikali na sekta binafsi wanatumia vyeti ambavyo siyo vyao.

Uchunguzi wa kina nilioufanya mwaka mmoja na miezi sita sasa umebaini kuwa waajiliwa hao hutumia vyeti na majina ambayo siyo yao kutokana na kugushi vyeti vya shule na vyuo kutokana na mfumo wa serikali kuajiri vyeti zaidi kuliko uwezo wa mtu kutokana na cheti chake.


Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa zaidi ya wanafunzi 264 waliofanya mtihani kidato cha sita Februari 2009 (ACSEE) walikuwa na sifa tata ambazo zilikuwa tayari zilikwisha tumiwa miaka mingine.


Sanjari na hayo uchunguzi huo umebaini pia kuwa wanafunzi 160 sifa zao zilikuwa tayari zipo kwenye orodha ya wanachuo waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Ualimu Daraja la A (GATCE) na Stashahada ya Ualimu (DSEE) Mei mwaka huu.


Sifa za wanafunzi hao ambao majina yao yanahifadhiwa, zimetumiwa na watahiniwa zaidi ya mmoja katika Shule/Vituo tofauti na wanachuo wanaoomba kufanya Mtihani wa Ualimu Daraja la A au Stashahada ya Ualimu mwezi Mei 2009 na baadhi sifa zao zilishatumiwa na watahiniwa wengine kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita miaka iliyopita.


Licha ya Baraza la mitihani nchini Necta kuwabaini baadhi ya waliogushi limeshindwa kuwachukulia hatua za kisheria ingawa baraza hilo linatambua kuwa ni kosa la jinai kughushi au kutumia cheti cha mtu mwingine.


Pamoja na kushindwa kuwachukulia hatua wanafunzi hao, baraza hilo limeweza kuwafikisha kinadhalia wanafunzi waliofanya mtihani wa Ualimu katika vyuo vya dola wanachuo 61 kutoka vyuo vya Ualimu ambao waliwasilisha nyaraka za kughushi au vyeti vya watu wengine kwa ajili ya uhakiki.


Vyuo ambavyo vinaelezwa kufanyiwa usahili wa vyeti na baraza hilo hapa nchini na kubaini wanafunzi waliogushi na idadi yao kwenye mabano waliofikishwa kwenye vyombo vya dola ni chuo cha Montessori (1), St Francis Nkindo (3), Kange (16), Eckenford (13), Sahare (7), Bukoba Lutheran (1), Mpuguso – Mbeya (2), Capital (6), Arafah (2), Arusha T.C (2), Greenbird (3), Tanzania College of Early Education (4) na Salesian Seminary (1).


Uhakiki huo ulifanywa kabla ya Mei 1 mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa baraza hilo linatarajia kufanya uhakiki mwingine zaidi kwa kutambua picha za wamiliki halali wa vyeti katika vyuo huku wengine wakiendelea kusoma na kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment