Friday, August 31, 2012

HAWA NDIO WACHEZAJI WA TANZANIA WALIOWEKEWA PINGAMIZI KUCHEZA LIGI KUU.

.
Klabu mbalimbali zimewasilisha pingamizi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga usajili wa wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu.

Toto Africans imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.
 
Pia Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.
 
Super Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne; Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya (African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.
 
Mchezaji Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.
 
Azam inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani. Nayo Simba inapinga Kelvin Yondani kusajiliwa Yanga kwa maelezo kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.
 
Vilevile Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na APR ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.
 
Nayo Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/2013.
 
Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano. Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.
 
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia pingamizi hizo pamoja na usajili wa wachezaji kwa ujumla kwa 2012/2013.
 
Redondo, Luhende, Christopher Edward, Kiggy Makasi na Yondani wawekewa pingamizi kucheza ligi kuu. (Stori imeandikwa na Shaffih Dauda wa shaffihdauda.com )

DC MBARALI MBEYA ANUSURIKA KUUMIZWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA UUGUZI CHIMALA

Na Venance Matinya, Mbeya.
MKUU wa Wilaya ya Mbarali Gulamu Hussen Kiffu  amenusurika kuumizwa na wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Chimala kilichopo Wilayani humo baada ya kuvamia gari lake na kuvunja vioo,kutoa upepo wa matairi  kutokana na Serikali kufunga chuo hicho kwa kutokuwa na hadhi ya kudaili wanafunzi.

Kutokana na vurugu hizo zilizotokea chuoni hapo juzi jioni, Jeshi  la polisi Mkoani Mbeya linawashikilia wanafunzi  sita    akiwemo Mkuu wa Chuo  hicho  Francis Mtega  kwa  tuhuma za kuhamasisha vurugu  zilizopelekea  kuharibu gari la Mkuu wa Wilaya ya  Mbarali. 

Kamanda wa polisi Mkoani hapa Diwani Athuman  alisema  baada ya mkuu wa wilaya kuongozana na baadhi ya viongozi wa serikali  hususani kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa lengo la kutaka kujua sababu za chuo hicho kuendelea kufundisha wakati serikali ilitoa agizo kifungwe ndipo hapo walipovamiwa na wanachuo hao.

Alisema   tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kuwasili Chuoni hapo kwa  lengo la  kuzungumza na uongozi wa chuo ndipo baadhi ya wanafunzi  walivamia gari la Mkuu wa Wilaya na kuanza kuvunja vioo kwa kutumia mawena kisha kutoa upepo kwa malengo yasiyojulikana.

Kamanda Athumani alisema tukio hilo linaonesha ni mpango uliokuwa umepangwa na uongozi wa Chuo  kwa muda mrefu kwani serikali ina malengo mazuri kwa watanzania  na lengo kuu ilitaka chuo hicho kisajiliwe  ili kitambulike  na Serikali na kuweza kutoa wauguzi walio na sifa na kuwawezesha kupata ajira itakayotambulika serikalini. 

Aliongeza kuwa  kitu cha kushangaza ni madaraka aliyonayo mkuu wa chuo hicho ambapo yeye mwenyewe ni mwalimu na mhasibu na kwamba kulikuwa hakuna sababu ya kufanya vurugu bali  kilikuwa ni kitu cha kutoa vielelezo vya udaili wa chuo.

Alisema katika uchunguzi wa awali  umebaini kuwa chuo hicho kimeanza muda mrefu na tayari  kimeweza kutoa wauguzi katika Nyanja mbalimbali  bila ya serikali kutambua  kama hakijasajiliwa na hakitambuliki.
  
“ Kutokana na vurugu hizo  wanafunzi  32 wanashikiliwa na Jeshi la P[olisi ambapo kati ya hao watano ndio waliobainika kuhusika na vurugu hizo na wanatarajiwa kufikiswa  mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazowakabili ili sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine” alisema Kamanda huyo.

Aliwataja  wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Mkuu wa Chuo  Francis Mtega, Steven Mapunda (19), Isaya Katuwa (23) , Lugano Mwalupasya (22), Emmanuel Bukuku (24)  ambao wanatarajia kufanya mtihani wiki ijayo ya kuhitimu mafunzo ya uuguzi. 

Kwa upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Mbarali  Gulamu Hussen Kiffu alikiri kutokea kwa vurugu hizo  zilizotokana na uamuzi wa serikali kufunga chuo hicho  kutokana na kutokuwa na sifa ya kufundisha na kudaili wanafunzi  wa fani ya uuguzi kwani kilikuwa hakina hati ya utambulisho wa usajiri serikalini.

Kiffu alisema kuwa baada ya serikali kutambua tatizo hilo ndipo walipo mwita  Mkuu wa Chuo  hicho Francis Mtega katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambapo aligoma kuhudhuria na kueleza kuwa yeye anaendelea kufundisha ndipo walipolazimika kufika chuoni hapo.

NDIMARA TEGAMBWAGE AKIWAKUMBUSHA WAANDISHI WA HABARI MAANA YA HABARI BORA

WANAFUNZI NA WAAJILIWA WENGI WANATUMIA VYETI VISIVYO VYAO.

* 264 Walifanya mtihani kidato cha sita Februari 2009 kwa kutumia sifa zilizowahi kutumiwa miaka iliyopita.

* 160 sifa za vyeti vyao zilitumiwa kujisajili na wanachuo wa ualimu daraja A na stashahada ya ualimu mei 2009.



WANAFUNZI wengi nchini hasa wa shule za Sekondari, vyuo na waajiliwa katika nafasi mbalimbali Serikali na sekta binafsi wanatumia vyeti ambavyo siyo vyao.

Uchunguzi wa kina nilioufanya mwaka mmoja na miezi sita sasa umebaini kuwa waajiliwa hao hutumia vyeti na majina ambayo siyo yao kutokana na kugushi vyeti vya shule na vyuo kutokana na mfumo wa serikali kuajiri vyeti zaidi kuliko uwezo wa mtu kutokana na cheti chake.


Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa zaidi ya wanafunzi 264 waliofanya mtihani kidato cha sita Februari 2009 (ACSEE) walikuwa na sifa tata ambazo zilikuwa tayari zilikwisha tumiwa miaka mingine.


Sanjari na hayo uchunguzi huo umebaini pia kuwa wanafunzi 160 sifa zao zilikuwa tayari zipo kwenye orodha ya wanachuo waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Ualimu Daraja la A (GATCE) na Stashahada ya Ualimu (DSEE) Mei mwaka huu.


Sifa za wanafunzi hao ambao majina yao yanahifadhiwa, zimetumiwa na watahiniwa zaidi ya mmoja katika Shule/Vituo tofauti na wanachuo wanaoomba kufanya Mtihani wa Ualimu Daraja la A au Stashahada ya Ualimu mwezi Mei 2009 na baadhi sifa zao zilishatumiwa na watahiniwa wengine kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita miaka iliyopita.


Licha ya Baraza la mitihani nchini Necta kuwabaini baadhi ya waliogushi limeshindwa kuwachukulia hatua za kisheria ingawa baraza hilo linatambua kuwa ni kosa la jinai kughushi au kutumia cheti cha mtu mwingine.


Pamoja na kushindwa kuwachukulia hatua wanafunzi hao, baraza hilo limeweza kuwafikisha kinadhalia wanafunzi waliofanya mtihani wa Ualimu katika vyuo vya dola wanachuo 61 kutoka vyuo vya Ualimu ambao waliwasilisha nyaraka za kughushi au vyeti vya watu wengine kwa ajili ya uhakiki.


Vyuo ambavyo vinaelezwa kufanyiwa usahili wa vyeti na baraza hilo hapa nchini na kubaini wanafunzi waliogushi na idadi yao kwenye mabano waliofikishwa kwenye vyombo vya dola ni chuo cha Montessori (1), St Francis Nkindo (3), Kange (16), Eckenford (13), Sahare (7), Bukoba Lutheran (1), Mpuguso – Mbeya (2), Capital (6), Arafah (2), Arusha T.C (2), Greenbird (3), Tanzania College of Early Education (4) na Salesian Seminary (1).


Uhakiki huo ulifanywa kabla ya Mei 1 mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa baraza hilo linatarajia kufanya uhakiki mwingine zaidi kwa kutambua picha za wamiliki halali wa vyeti katika vyuo huku wengine wakiendelea kusoma na kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

JIJI LA MBEYA LALALAMIKIWA ''UFISADI'' ARDHI

* Afisa anayelalamikiwa ahamishwa badala ya kuwajibishwa
 
SIKU chache baada ya wananchi wa Jiji la Mbeya kuwalalamikia baadhi ya maafisa Ardhi wa Jiji hilo kujikadilia mapato kidogo ya nyumba zao huku wakiwapandishia gharama wananchi wa kawaida, tuhuma zingine nzito za uporaji wa ardhi zimeibuka dhidi yao huku wakidaiwa kuendelea kulindwa.
 
Hali hiyo imebainika baada ya wananchi hao kumwandikia barua Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya makazi huku wengine wakimwandikia Meya wa Jiji hilo Athanas Kapunga kuwalalamikia maafisa wa Jiji la Mbeya kuwapora ardhi kwa mgogo wa Serikali kuchukua ardhi hiyo kwa matumizi maalum.
 
Barua ambazo zimenaswa na kuthibitishwa ni pamoja na barua ya wananchi wakazi wa mtaa wa Manga Veta kata ya Ilemi Mbeya Mjini ambao wamepeleka kero Wizarani na ofisi ya Rais –Ikulu kwa kile walichodai kuwa ni vitendo wanavyofanyiwa na ofisi ya Ardhi Jiji la Mbeya.
 
Barua hiyo ya Agosti 9,2011 imesema kuna mchezo mchafu umekithiri kwa watendaji wa Jiji la Mbeya kitengo cha ardhi ambao hujimilikisha maeneo kwa kutumia majina hewa kumbe viwanja hivyo ni vyao wenyewe na wakiulizwa wanasema kuwa ni sheria za mipango miji.
 
‘’Tuliletewa barua tarehe 13.06/2011 yenye kumb.Na. MCC/LD/M.13/VOLI. Iliyoandikwa na mwanasheria wa Jiji S.W.Mwangomale akishirikiana na mthamini wa Jiji Bi. Edina Mwaigomole akituamuru kuondoka eneo hilo ndani ya siku 14 wakidai kuwa Serikali imetenga eneo hilo kwa ajili ya soko wakati si kweli’’ imesema moja ya haya ya barua hiyo.
 
Barua hiyo imeendelea kusema kuwa katika barua hiyo ilionekana kuwa wananchi walikuwa tayari wamelipwa wakati hakuna mkutano wowote uliowahi kufanyika kwa ajili ya makubaliano ya kuondoka eneo hilo ambapo wananchi wameomba kuthibitishwa na kuoneshwa mtiririko wa malipo kutoka ofisi ya Jiji hali ambayo mpaka sasa imeshindikana kuthibitishwa.
 
Baada ya malalamiko ya wananchi, Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia barua ya Juni 25, 2012 yenye kumb.Na. EA 71/176/01H  iliyosainiwa na Kaimu katibu wa Wizara hiyo Verdiana A. Mashingia ilisema kuwa inashughulikia malalamiko hayo.
 
Wakati wananchi wa eneo hilo wakilalamikia idara hiyo ya Ardhi, wakazi wengine wa eneo la Gombe kusini kata ya Itezi jijini humo wameamua kumwandikia barua ya malalamiko Mstahiki Meya wa Jiji hilo wakiwalalamikia maafisa wa idara hiyo ya ardhi kuwa maeneo yao yameuzwa kwa watu wengine ili hali kuna nyumba zao za kuishi.
 
Barua hiyo ambayo imeandikwa Agosti 16, 2012 iliambatanishwa na nyaraka mbalimabli za mawasiliano na idara ya mipango miji na historia ya eneo hilo huku wakilalamikia pia matumizi mabaya ya madaraka na sheria kwa kujinufaisha nazo zinazowawezesha kuhalalisha ubovu na ubinafsi katika utendaji.
 
‘’Kupima maeneo ambayo tayari yamejengwa na kuwapa hati watu wengine na hivyo kuwaondoa wakazi asili kiuonevu kwa kuwa hawana uwezo kifedha na zoezi kunuka rushwa waziwazi. Kwa mfano kamati zikibatilisha na kubadili matumizi ya ardhi, maofisa wanakaa kwa nia ya kujinufaisha na kupanga watekeleze vipi na kwa kiwango gani’’zimesema haya za barua hiyo yenye kurasa tatu.
 
Eneo hilo ambalo lipo karibu na shule za St. Agrrey awali lilipangwa kuwa eneo la viwanda lakini likabadilishwa kuwa makazi ya watu lakini inaonekana kuwa baadhi ya maafisa ardhi (majina yanahifadhiwa) wanahusika kulihujumu.

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Idd alisema kuwa kuhusu suala la eneo la Manga analifahamu na analitafutia ufumbuzi kwasababu malalamiko ya wananchi ameyapokea na suala la Gombe kusini ameahidi kulitolea majawabu hapo baadae huku akisema kuwa Afisa Ardhi anayelalamikiwa amehamishwa.

WANAWAKE MBEYA WATAHADHARISHWA NA PEDI FEKI

  Hii bidhaa baadhi ya kina mama wameilalamkia haina ubora na inawatoa vidonda hatujapenda kutoa picha za akina mama hao walioleta ila zipo na kila mhusika tukimuuliza anasema watu wa viwango ndiyo wanahusika sasa mbeya hakuna ofisi za viwango je wafanyeje akina mama hao waliopata matatizo?

WANAWAKE mkoani Mbeya wanapaswa kujihadhari na bidhaa feki wanazotumia hasa za kujisitiri wakati wa siku zao (hedhi).

Uchunguzi uliofanywa na kuthibitishwa na baadhi ya wanawake umebaini bidhaa hizo feki zimekuwa zikiwavimbisha wanawake pindi wanapozitumia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema uwepo wa bidhaa zisizothibitishwa viwango vya ubora kwa kiasi kikubwa inachangiwa na kukosekana kwa ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Walibainisha kuwa hali hiyo imechangia bidhaa nyingi zinazoingia mkoani Mbeya kupitia mipaka ya Kasumulu kwa upande wa nchi ya Malawi na Tunduma kwa upande wa Tanzania kuwafikia walaji na watumiaji bila ya kukaguliwa ubora wake, hali ambayo ni hatari kwa afya zao.

Aidha, mmoja wa wamiliki wa viwanda vya kuzalisha mafuta ya alizeti kwenye soko la Sido eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya, Sophia Adamu, alisema hakuna ukaguzi wowote unaofanywa na TBS kwa mafuta yanayozalishwa kwenye viwanda vyao na kupelekwa moja kwa moja kwa walaji bila ya kuthibitishwa ubora wake na shirika hilo.

Alisema tangu ameanza kufanya biashara hiyo hajawahi kuwaona TBS wakienda kukagua bidhaa zao na kuthibitisa ubora na akashauri shirika hilo kufungua matawi mikoni hususan Mkoa wa Mbeya ambao una viwanda vingi vidogo vidogo.

KUTANA NA WAHUBIRI WATOTO WANAO CHAPA INJILI, WANAWEZA KUSIMIKWA KUWA WACHUNGAJI?

Mamake Ezekiel na babake wa kambo ni wachungaji wa kanisa la 'Fullness of time' huko Maryland kanisa ambalo walilianza miaka miwili iliyopita.Ni katika kanisa hili ambapo hezekaiah alitawazwa kuwa mchungaji na ndugu yake shemasi mapema mwaka huu.

'Ulikuwa wakati wa ajabu kwangu' alisema Hezekiah nduguye Ezekiel mwenye umri wa miaka 13.'Kila mtu kanisani alitupigia makofi kwa furaha na kutupongeza'

Micah, nduguye Hezekiah ana umri wa miaka saba na tayari anataka kufuata nyayo zake hezekaih 'Tayari nimetayarisha mahubiri lakini nitayahubiri nitakapo hitimu miaka 10' alisema Micah kwa sauti ya unyenyekevu.

Sio nchi ya marekani tu ambayo ina watoto wanaohubiri, bali Brazil pia imeboboea katika jambo hili.Indonesia pia haijawachwa nyuma kwani ina kipindi cha runinga ambacho wahubiri wachanga wa dini ya kiislamu hishindana. ini se

'Jambo hili lina uwezo wa kuchipuka haswa katika dini ambazo husisistiza uwepo ya roho mtakatifu na pia jamii zilizotengwa' asema Edith Blumhofer mtaalam wa historia ya wakristo chuo cha Wheaten mjini Illinois.

Ted Lavigne kasisi aliye staafu na anaandika kitabu kilicho na mada hii ya watoto wahuburi,asema kuwa wahubiri wengi watoto walisikika sana miaka ya 1920 na 1930 wakati ambapo kanisa la pentekoste lilikuwa changa.


Fasihi za awali zinaelezea wakati huu ambapo watoto walisikika wakinena maneno yenye hekima kuliko miaka yao.Jambo hili lilipokelewa kwani lilikuwa thibitisho la uwepo wa Roho Mtakatifu.
Jambo la kushangaza ni kwamba,jinsi makanisa haya yalipoendelea kuwatumia watoto hawa ndivyo waliendelea kuonekana wamejitenga.

Lavigne amegundua takriban mifano 500 tangu miaka ya 1500 na 1700 ya watoto hawa,wengi wao wakiwa na asili ya marekani na wengine uingereza.

'Kuna elimu ya nguvu ya kidini inayoendelea hapa nchini.Hapa Amerika kuna watu wanaopeda dini sana' asem Randall Balmer mwenyekiti wa kitengo cha dini chuo cha Dartmouth.
Waumini kanisani


Kanuni zinazosema nani anayeweza kuanzisha kanisa zina posho kubwa kwa hivyo mtu yeyote anaweza kuanzisha kanisa mahali popote.Kanisa la familia ya Ezekiel ni kanisa ambalo halifuati madhehebu yoyote kwa hivyo wana uhuru wa kufanya mambo yao vyovyote.

Hata hiyo si vigumu kupata watu walio na wasiwasi kuhusu watoto wahubiri.Watu kama hawa huwa na dhana kuwa ni wachanga sana kuapishwa kama kasisi na wana ushahidi wa kesi za watoto wahubiri waliopotoka.

Ushahidi mkubwa haswa ni ule wa Marjoe Gortner,mtoto mhubiri aliyetangaza baada ya miaka mingi kuwa hakuamini kuwa kuna Mungu na alikuwa mhubiri kwa shinikizo ya wazazi wake na baadaye kama ajira.

Wazazi wa Ezekiel wanafahamu fika mambo haya na wako tayari kumtetea mtoto wao.Mamake asema kuwa watoto wake wana adabu na tabia nzuri.Maisha ya watoto wao ina uwianao,kwani hata ingawa ni wahubiri wao kufanya vitu ambavyo watoto wa kawaida hufanya kama kwenda shule,kucheza na watoto wengine na kadhalika.

Hata hivyo watoto hawa hukumbwa na changamoto nyingi kwa sababu ya majukumu yao ya kuhubiri.Kwa mfano ,wao hufanya masomo nyumbani kwa vile wakienda shuleni hutaniwa wenzao.

Ezekiel bado hajaamua kazi atakayoifanya maishani. Hajaamua kama atakuwa mhubiri maisha yake yote ama ataifanya kazi ingine.


Siku hizi watoto wanao hubiri ni wachache nchini amerikani na amabao wako,huhubiri kwenye mitaa.


Source:Martblog

KUTOKA ZANZIBAR

 MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada Rai (kushoto) akimkabidhi shahada ya uzamivu (PHD)  ya Heshima ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.Rais mstaafu wa awamu ya tano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Dk.Salmin Amour Juma nyumbani kwake Migombani mjini Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein).


 
RAIS Mstaafu wa Zanzibar,Dk.Salmin Amour Juma katikati akizungumza na Viongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) mara baada ya kumkabidhi shahada ya Uzamivu (PHD) ya Heshima ya chuo hicho,kushoto Makamu Mkuu wa SUZA,Prof.Idris Ahmada Rai  na Mjumbe wa Baraza la Chuo Mohammed Said Dimwa,katika makaazi ya Rais huyo Migombani mjini Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein).

Wednesday, August 29, 2012

WHAT ARE SOCIAL NEWS ?


A social news website features user-posted stories that are ranked based on popularity. Users can comment on these posts, and these comments may also be ranked. Since their emergence with the birth of web 2.0, these sites are used to link many types of information including news, humor, support, and discussion. Social news relies on crowd sourcing to shape focus in a bottom-up fashion, forming a type of collective intelligence. Social news sites facilitate democratic participation on the web.[c

Websites
Slashdot
Slashdot, started in 1997, was one of the first social news websites. It focuses mainly on science and technology related news. Users can submit stories, and the editors pick out the best stories each day for the front page. Users can then post comments on the stories.[1] The influx of web traffic that resulted from Slashdot linking to websites led to the effect being coined as the Slashdot effect.
Fark
Fark was started in 1997, and featured news of any topic. On Fark, users can submit articles to the administrators of the site. Each day, these administrators pick out 50 articles to display on the front page.[2]
Delicious
Delicious, started in September 2003, is a social news website which allows users to create a profile, and then use that profile to create "stacks". Stacks are what delicious.com refers to as a "playlist to the Internet". Essentially, users find links to different webpages or media that relate to a common theme or topic. Stacks must have at least three links in order to become a published work. Featured articles are chosen by the publishers of the website and showcased on the homepage of delicious. As of December 2011, delicious.com includes subcategories in which each stack may be categorized. [3]